
Yanga SC imeshindwa kuondoka na ushindi mbele ya Al Ahly ya Misri baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) uliopigwa leo Januari 31, 2016 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, kikosi cha Wananchi kilitangulia kupata bao la uongozi kupitia beki wake wa kati, Ibrahim Bacca, aliyetikisa nyavu katika kipindi cha kwanza na kuwapa matumaini mashabiki wa Yanga.
Hata hivyo, Al Ahly walirejea kwa nguvu kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao kupitia kiungo wao wa kati raia wa Mali, Diening, aliyefunga kwa mpira wa kona uliokufa na kurejesha mchezo katika usawa.
Matokeo hayo yanaiweka Yanga katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi ikiwa na pointi tano (5), huku Al Ahly wakiendelea kushikilia nafasi ya juu kwa kujikusanyia pointi nane (8).

Social Plugin