Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA TAN) imeishukuru kampuni ya mabasi ya Ally’s Star kwa kutoa huduma bora zenye viwango vya kimataifa.
Mwenyekiti wa MISA TAN, Bwana Edwin Soko, ametoa shukrani hizo za dhati kupitia kwa Meneja wa kampuni hiyo, Bwana Ally Salumu.
Soko amesema kuwa pongezi hizo hazikuwa tu za maneno bali za kujionea, kwani kampuni ya Ally’s Star iliwasafirisha wahariri na waandishi wa habari wanachama wa MISA TAN kutoka mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza na Shinyanga kuelekea mkoani Iringa kuhudhuria Mkutano wa MISA Wadau Summit 2026 na Mkutano Mkuu wa MISA TAN.
Safari hiyo ilihakikishwa kwa usalama na huduma ya hali ya juu kwa muda wote.
Aidha, Soko ameongeza kuwa mabasi ya Ally’s Star yalitoa huduma bora zenye viwango vya kimataifa, ikiwemo punguzo la bei kwa kuenzi mchango wa waandishi wa habari katika sekta ya usafirishaji, pamoja na viburudisho na burudani kwa muda wote wa safari.





Social Plugin