Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yudas Ndungile, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akifuatiwa na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia. Picha na Kadama Malunde

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment - MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog
Shirika la Tanzania Health Promotion Support limekabidhi rasmi Kliniki mpya ya Tiba ya MAT (Medically-Assisted Treatment) katika Manispaa ya Shinyanga kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha juhudi za kukabiliana na changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Kliniki hiyo imejengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB wenye thamani ya shilingi milioni 145, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya pamoja ya kuboresha afya na ustawi wa jamii za Watanzania, hususan vijana. Kliniki hii imejengwa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, DCEA, pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, kwa kuzingatia viwango vya kitaifa.
Kituo hicho kimepokelewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika Jumapili Machi 22, 2026.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amelipongeza Shirika la THPS na CRDB Bank kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha ujenzi wa kituo hicho, akisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya kweli ya wadau kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na dawa za kulevya.
“Nalipongeza Shirika la THPS kwa hatua hii muhimu inayoongeza nguvu katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya. Pia naishukuru Benki ya CRDB kwa msaada wao mkubwa. Nawahimiza wananchi, hususan vijana walioathirika, kutumia huduma hizi ili kwa pamoja tulinde afya na mustakabali wa jamii zetu,” amesema Lyimo.
Aidha, ametoa wito kwa taasisi nyingine za fedha na sekta binafsi kuiga mfano wa Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto za kijamii, akibainisha kuwa mchango huo umeokoa rasilimali za Serikali na kuboresha moja kwa moja afya ya wananchi.
Amesisitiza kuwa kupanua upatikanaji wa huduma za matibabu ni nguzo muhimu katika mkakati wa Tanzania wa kupunguza madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya na kuhamasisha uponaji.
Amesema ujenzi wa kliniki hiyo unaonesha umuhimu wa ushirikiano madhubuti kati ya serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi katika kukabiliana na changamoto za afya ya umma.
Kamishna Lyimo amesema kituo hicho kipya kitatoa huduma za bure, zenye ushahidi wa kisayansi kwa watu wanaokabiliwa na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya, ikiwemo tiba ya MAT, ushauri nasaha pamoja na msaada wa kisaikolojia na kijamii.
"Kupitia tiba ya Methadone inayotolewa kwa utaratibu maalum pamoja na huduma jumuishi, wapokea huduma watawezeshwa kudhibiti uraibu, kupunguza hatari za kiafya na kurejea katika maisha ya kawaida ya kijamii",ameeleza.

Amesema hadi sasa, kuna kliniki 22 za MAT nchini nyingi zikiwa katika hospitali za rufaa za mikoa, na kuanzishwa kwa kliniki ya Shinyanga kunaongeza upatikanaji wa huduma hizi muhimu katika mkoa huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia, amesema kabla ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo, waraibu wengi wa dawa za kulevya kutoka Shinyanga walilazimika kusafiri hadi Mkoa wa Mwanza kupata matibabu, hali iliyosababisha baadhi yao kushindwa kufikia huduma hizo kwa urahisi.
Mkurugenzi wa THPS Dkt. Redempta Mbatia (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya MAT Shinyanga.
Dkt. Redempta ameeleza kuwa ndipo walipoamua kuomba ufadhili kutoka CRDB Bank ili kujenga kituo hicho, ambacho sasa ni cha kwanza cha aina yake katika Mkoa wa Shinyanga.
“Tunajivunia kuona jitihada hii muhimu ikifanikiwa. Naishukuru Benki ya CRDB kwa msaada wao na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake endelevu. Huu ni mfano mzuri wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuimarisha upatikanaji, usawa na ubora wa huduma za afya, sambamba na ajenda ya Uhakika wa Afya kwa Wote,” amesema Dkt. Redempta.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid M. Nsekela, amesema benki hiyo ina utaratibu wa kutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi (VAT) kwa ajili ya kurejesha kwa jamii kupitia miradi ya afya, elimu, mazingira na maeneo mengine ya kijamii.
“Benki ya CRDB inathamini ushirikiano wake na THPS pamoja na Serikali ya Tanzania na zaidi niwapongeza THPS ambao walileta kwetu wazo hili na sisi tukafanya ufadhili huu. Kusaidia ujenzi wa kliniki hii ni kielelezo cha dhamira yetu ya kuboresha ustawi wa jamii tunamofanya biashara na kuifanya benki ya CRDB kuwekeza kwa jamii badala ya kufanya biashara pekee. Tukiwa kama benki kiongozi nchini Tanzania, tutaendelea kuunga mkono programu zenye matokeo chanya na endelevu kwa jamii,” amesema Wagana.
“Huu ni mwendelezo na tunaahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kusaidia miradi ya serikali. Tunaamini katika mashirikiano ya Serikali na sekta binafsi ndo chachu ya mafanikio katika maendeleo. Mwisho tunawaomba wadau wote – wafanyakazi, wafanyabiashara, wastaafu, vijana, na makundi yote – kuendelea kutumia huduma za CRDB nchini Tanzania ili asilimia moja baada ya kodi iweze kuongezeka na kusaidia maeneo mbalimbali yenye uhitaji”,ameongeza Wagana.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, amesema tayari maandalizi muhimu yamekamilika ikiwemo upatikanaji wa watumishi wa afya, samani za kliniki pamoja na maboresho ya mazingira ya kituo hicho ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa kwa ufanisi.
Aidha, ameomba wadau kuendelea kuunga mkono kituo hicho kwa kukiwezesha kupata vifaa muhimu zaidi ikiwemo mashine za kupima kiwango cha matumizi ya dawa (meter measure) ili kusaidia kupanga dozi sahihi kwa wagonjwa kulingana na kiwango cha uathirika.

Kuhusu THPS
Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa nchini Tanzania na kusajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002, lenye dhamira ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa Watanzania wote.
Tangu mwaka 2011, THPS imekuwa ikishirikiana wa Serikali ya Tanzania katika kuimarisha mifumo ya afya na jamii—kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yale yamlipuko, magonjwa yasiyoambukiza, afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga, vijana na watoto, pamoja na kuondoa vikwazo vya kimuundo katika upatikanaji wa huduma za afya.
Kupitia ushirikiano wa kimkakati na mbinu zinazotokana na utafiti wa kisayansi, THPS inaendelea kuchangia katika maboresho ya afya endelevu na kushirikiana katika kuandaa na kutathmini afua za afya ya umma.
Kuhusu Huduma za tiba kwa waraibu (MAT)
Huduma za MAT ni huduma za afya zinayolenga watu wanaotumia dawa za kulevya, hasa wanaotegemea dawa za kulevya aina ya opioidi kama heroini.
Huduma hii hutumia mchanganyiko wa dawa maalum, ushauri nasaha na tiba ya kisaikolojia ili kusaidia watu kuacha au kupunguza matumizi ya dawa hatarishi na kuimarisha afya zao.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment - MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, pamoja na Mkurugenzi wa Tanzania Health Promotion Support, Redempta Mbatia. Picha na Kadama Malunde
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia (wa pili kulia) akizungumza wakati Uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia (wa pili kulia) akizungumza wakati Uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kliniki ya MAT iliyojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akifuatiwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi. Wa kwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, pamoja na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akipata maelezo kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa katika Kliniki ya MAT kutoka kwa mtaalamu wa afya.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akipata maelezo kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akitembelea Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akielezea kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment - MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kuhusu umuhimu wa huduma za MAT katika kupambana na uraibu wa dawa za kulevya.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kuhusu umuhimu wa huduma za MAT katika kupambana na uraibu wa dawa za kulevya.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akielezea namna huduma zitakavyotolewa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akielezea namna huduma zitakavyotolewa.
Kamishna wa Kinga na Tiba wa DCEA, Dkt. Peter Patrick Mfisi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mnufaika wa huduma za MAT, Ibrahim Seif akieleza jinsi alivyofanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya miaka 10.
Mnufaika wa huduma za MAT, Ibrahim Seif akieleza jinsi alivyofanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya miaka 10.


Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

Picha ya pamoja ya Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, viongozi mbalimbali na wanufaika wa huduma za MAT.
Picha ya pamoja Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo , viongozi mbalimbali pamoja na maafisa wa Benki ya CRDB na THPS.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
















































Social Plugin