
Daraja la Mto Ruwembe lililopo Mikumi na linalounganisha Mji wa Mikumi na eneo la Ifakara limekatika leo alfajiri kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwandishi wa habari aliyepo eneo la tukio ameshuhudia uharibifu wa daraja hilo uliosababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Mikumi na Ifakara, ambayo ni njia muhimu inayotumiwa na wakazi pamoja na wafanyabiashara katika ukanda huo.
Kutokana na hali hiyo, shughuli za usafiri na usafirishaji zimesimama kwa muda katika barabara hiyo huku wananchi wakilazimika kusubiri hatua zaidi za mamlaka husika.
Kwa sasa, vyombo vya uokoaji na usalama vimefika katika eneo la tukio na vinaendelea na jitihada za kuhakikisha usalama wa wananchi pamoja na watumiaji wa barabara hiyo muhimu kwa shughuli za kiuchumi za wakazi wa maeneo hayo.
Social Plugin