Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC MTATIRO AAGIZA TATHMINI YA NYUMBA ZILIZOJENGWA ENEO LA MWEKEZAJI BUTENGWA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julias Mtatiro akisikiliza kero za wananchi  ambao wameeleza changamoto mbalimbali zilizopo kwenye mitaa yao ikiwemo migogoro ya ardhi

 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza na wananchi wa Butengwa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakati wa kusikiliza kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza na viongozi kwa njia ya simu ambao wako safarini.
Na Stella Herman, Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro amefanya ziara katika Kata ya Ibinzamata na Ndembezi kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi na kuchukuwa hatua ili kuondoa changamoto hiyo na kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya amesema migogoro ya ardhi inachelewesha maendeleo kutokana na wananchi kushindwa kuyaendeleza maeneo yao na kutumia muda mrefu kutatua migogoro ya ardhi.

Amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata taratibu za kununua viwanja kupitia idara ya ardhi ili kuepuka kuuziwa viwanja na matapeli ambao wanatambua eneo linamgogoro lakini bado wanawauzia wananchi kitendo ambacho kinachochea migogoro.

“Unajenga kwenye eneo ambalo unajua Tanesco hawataleta umeme,Shuwasa hawataleta maji na huduma zingine za kijamii matokeo yake mnaanza kuilaumu serikali haiwajali wananchi kufikisha huduma za kijamii wakati mkijua kabisa maeneo yenye mgogoro serikali haipeleki huduma”amesema Mtatiro
Amesema eneo la Butengwa nila mwekezaji Kaseki ambaye ndiyo mmiliki tangu mwaka 1994 lakini limevamiwa na wananchi na kuanza kujenga makazi jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu kutokana na viongozi wa maeneo husika ngazi ya mtaa kushiriki katika kuchangia kukuza mgogoro huo

Kutokana na changamoto hiyo Mkuu wa Wilaya amewaagiza watendaji wa Mitaa kufanya thimini ili kujua idadi ya nyumba zilizojengwa katika eneo hilo na ziko katika hatua gani ili kuona namna ya kumaliza mgogoro huo kupitia mkutano utakao jumuisha wananchi,watalaam wa halmashauri na mwekezaji wa eneo.


Mwananchi mkazi wa Butengwa akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro nyaraka ya umiliki wa kiwanja katika eneo la Bitengwa ambalo linamgogoro kati ya wananchi na mwekezaji





Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akiangali ramani ya eneo lenye mgogoro akiwa na wananchi na watalaam kutoka idara ya ardhi


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akiangali ramani ya eneo lenye mgogoro akiwa na wananchi na watalaam kutoka idara ya ardhi























Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com