Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MICHEZO YA RIADHA NA WAVU YAWA KIVUTIO BONANZA LA MICHEZO PLUS

 



Na Oscar Assenga, TANGA

BONANZA la Michezo maarufu kama Michezo Plus limekuwa na mvuto wa aina yake huku likifanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Tanga Ufundi kwa kushirkisha wanafunzi zaidi ya 500.

Wanafunzi hao kutoka shule 50 Jijini Tanga ambao walishiriki katika Michezo ya Riadhaa na Wavu ambayo ilionekana kuwa kivutio kikubwa kutokana na namna washiriki wake walivyokuwa wakicheza kwa umakini mkubwa.

Bonanza hilo pia lilishiriki michezo mingine ikiwemo mpira wa Miguu,Pete  huku wakionyesha vipaji vya hali ya juu hatua iliyoshangiliwa na wadau wa michezo ambao walijitokeza kushuhudia bonanza hilo

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Bonanza hilo Afisa Michezo wa Jiji la Tanga na Mratibu wa Michezo Plus katika mradi unaotekelezwa na Jiji hilo ukifadhiliwa nan a Botnar Foundation chini ya Programu ya Tanga Yetu Lucy Michael alisema kwamba waliliandaamaalumu kwa ajili ya kujenga mahusiano na kuwajenga kiakili.

Alisema kwamba bonanza hilo litakuwa linafanyika kila mwaka mara mbili ambapo hilo limeanza kwa kufungua mwaka na kukaribisha wanafunzi na watafanya bonanza la vijana.

Awali akizungumza Mratibu wa Bonanza hilo Haji Milao alisema kwamba nia na madhumuni yake ni kuwaweka watoto sawa kwa ajili ya michezo ya Umistashumta mwaka huu 2026 ikiwemo kutengeneza afya za watoto ili waweze kuwa sawa na watoto wakiwa vizuri kwenye michezo hata darasani watakuwa vizuri.



Naye kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Makorora Zuhuru Ally alisema michezo hiyo ina faida kubwa sana kwao kutokana na kwamba inawafanya wakutana na wenzao na kubadilisha mawazo jambo ambalo linawapa fursa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com