Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE) kwa mwaka 2025, ambapo Shule ya Sekondari Little Treasures, iliyopo Manispaa ya Shinyanga, imeibuka kuwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri kitaifa.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na NECTA, shule hiyo imesajili jumla ya watahiniwa 60, kati yao 57 wamepata Daraja la Kwanza (Division I) huku wanafunzi 3 wakipata Daraja la Pili (Division II). Hakuna mwanafunzi aliyepata Daraja la Tatu, la Nne wala kufeli, jambo linaloonesha kiwango cha juu cha ufaulu na ubora wa maandalizi ya kitaaluma shuleni hapo.
Katika mgawanyo wa kijinsia, wanafunzi wa kike 25 wote wamepata Daraja la Kwanza, huku upande wa wavulana ukiwa na 32 waliopata Daraja la Kwanza na 3 Daraja la Pili, matokeo ambayo yanaakisi usawa wa kijinsia katika ufaulu na nidhamu ya masomo.
Aidha, takwimu za ufaulu wa masomo zinaonesha kuwa wanafunzi wa Little Treasures Secondary School wamefanya vizuri katika masomo mbalimbali ikiwemo Hisabati, Sayansi, Kiingereza na masomo ya jamii, yakionyesha ufanisi wa walimu, usimamizi madhubuti wa shule pamoja na mazingira bora ya kujifunzia.
Wadau wa elimu katika Manispaa ya Shinyanga wamepongeza uongozi wa shule, walimu, wanafunzi pamoja na wazazi kwa matokeo hayo, wakieleza kuwa mafanikio hayo ni kielelezo cha uwekezaji sahihi katika elimu na ushirikiano mzuri kati ya shule na jamii.
Matokeo kamili ya shule hiyo yanapatikana kupitia tovuti rasmi ya NECTA:
👉 Matokeo ya Kidato cha Nne Little Treasures Secondary
Social Plugin