RC MACHA ATEMBELEA BANDA LA CHUO CHA AFYA KOLANDOTO - AFYA CODE CLINIC

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia mwenye shati jeupe) akiwa katika Banda la Chuo cha Sayansi Kolandoto kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Julai 25,2024 wakati akifungua rasmi Kampeni ya Afya Code Clinic inayofanyika katika viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga inayoendeshwa na Jambo Fm Radio kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga kinashiriki Maonesho ya Afya Code Clinic kwa kutoa Huduma za maombi ya kujiunga na Chuo hicho kwa kozi za Afya zikiwemo Radiology, Physiotherapy, Clinical Medicine,Pharmaceutical Sciences, Medical Laboratory, Nursing & Midwifery na Kozi za Ufundi zikiwemo Maabara za Viwanda na Kompyuta. Pia wanatoa Huduma za Kupima Uzito na Urefu, Malaria (Zote Bure) lakini pia ukiwa katika Banda hilo utashuhudia mfano wa Leba jinsi Mama Mjamzito anavyojifungua. PICHA ZOTE NA KADAMA MALUNDE - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia) akiwa katika Banda la Chuo cha Sayansi Kolandoto

soma pia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post