DK. MWINYI AWATEMBELEA BORAAFYA, MZEE KOMBO NA HAJI RAMADHAN BAADA YA SALA YA IJUMAA

Na Mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Miembeni, Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Rais Dk. Mwinyi baada ya sala ya Ijumaa amewatembelea Wazee  na kuwajulia hali wakiwemo Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Mjini Boraafya Silima  nyumbani kwake Mwembeshauri, Kombo Mzee Kombo nyumbani kwake Miembeni Jitini pamoja na Haji Ramadhan Suwedi Mwandishi mwandamizi mstaafu wa ZBC na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Zanzibar aliyelazwa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post