MWALIMU AUAWA KWA KUCHOMWA KISU SHULENI



Mwalimu mmoja ameuawa na watu wawili wamejeruhiwa vibaya katika shambulio la kisu katika shule moja nchini Ufaransa, maafisa wanasema.

Waziri wa mambo ya ndani Gérald Darmanin amesema shambulio hilo lilitokea katika shule ya sekondari ya Gambetta katika mji wa kaskazini wa Arras mwendo wa saa 11:00 kwa saa za eneo hilo.

Mshambuliaji huyo amekamatwa na sasa anazuiliwa.

Kwa mujibu wa mashahidi, alipiga kelele "Allahu Akbar", au "Mungu ni mkuu", wakati wa shambulio hilo.Mtu aliyeuawa alikuwa mwalimu wa lugha ya Kifaransa. Waliojeruhiwa ni mwalimu mwingine na mlinzi.

Mtu huyo, anayetajwa kuwa na umri wa miaka 20, ana asili ya Chechen na anajulikana kwa idara za usalama kwa kuhusika kwake na Uislamu wenye msimamo mkali, kwa mujibu wa polisi.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema kuwa alikuwa mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo.

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Ufaransa imesema imeanzisha uchunguzi kufuatia shambulio hilo la "kuhusika na biashara ya kigaidi" na "kujaribu mauaji kuhusiana na biashara ya kigaidi".

Kituo cha habari cha BFMTV kimeripoti kuwa ndugu wa mshambuliaji huyo pia amekamatwa na polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post