Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROF. JANABI AZINDUA WODI YA WATOTO NJITI HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA, MWANZA

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Prof. Mohamed Janabi amezindua wodi ya kwanza na ya kisasa nchini kwa ajili ya watoto njiti, iliyojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Prof. Janabi amefanya uzinduzi huo jumamosi Februari 28, 2028 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus ambapo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 2.125 ikijumuisha jengo, vifaa tiba na mbili nyumba za watumishi.

Prof. Janabi ametumia fursa hiyo kuipongeza taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation- DMF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Keep a Child Alive (KCA) na Shirika la JHPIEGO  kwa kufanikisha mradi huo utakaosaidia kuzuia vifo vya wazazi na watoto hasa wanaozaliwa kabla ya wakati ama chini ya uzito.

"Kila mwaka Kanda ya Afrika inapoteza watoto milioni hivyo WHO tutaendelea kuunga mkono jitihada hizi ili kuhakikisha hakuna mtoto ama mzazi anapoteza maisha" amesema Prof. Janabi huku pia akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada inazoendelea kuchukua kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuboresha huduma za afya.

Mkurugenzi wa DMF, Doris Mollel amesema wazo la ujenzi wa wodi hiyo lilianza mwaka 2021 taasisi hiyo ilipoenesha kampeni ya kuchangia vifaa tiba kwa ajili ya wodi za watoto njiti nchini ambapo Wilaya ya Kwimba ilibainika kuwa kwenye uhitaji wa wodi na hivyo kuanza mchangato wa kutafuta fedha zilizofanikisha kukamilisha mradi huo.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la JHPIEGO Tanzania, Alice Christensen amesema kukamilika kwa wodi hiyo kutatoa mfano kote nchini namna wodi za watoto njiti zinavyopaswa kuwa hatua itakayosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua ambapo shirika hilo limechangia zaidi ya shilingi milioni 200 kwenye utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Kwimba akiwemo Modesta Malashi, Vumilia Ally na Mariam Lucas wamesema wodi hiyo itawaondolea adha ya kubanana kwenye wodi ya pamoja iliyokuwepo awali hospitalini hapo huku pia wakilazimika kusafiri umbali mrefu hadi Bugando inapotokea changamoto ya kujifungua.
Na George Binagi, Mwanza
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi (wa tano) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la wodi ya watoto wachanga waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza iliyojengwa na taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la JHPIEGO na Taasisi ya Keep a Child Alive. Profesa Janabi amefanya uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi (mwenye kofia) akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa jengo la wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza iliyojengwa na taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la JHPIEGO na Taasisi ya Keep a Child Alive. Profesa Janabi amefanya uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi (mwenye kofia) akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa jengo la wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza iliyojengwa na taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la JHPIEGO na Taasisi ya Keep a Child Alive. Profesa Janabi amefanya uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus.
Viongozi na wadau mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza ambayo imegharibu shilingi bilioni 2.125 ikijumuisha jengo, vifaa na nyumba za watumishi. Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi amefanya uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus kwenye hafla ya uzinduzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Afya, Florence Samizi akizungumza uzinduzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.
Mkurugenzi Shirika la JHPIEGO Tanzania, Alice Christensen akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation (DMF), Doris Mollel akizungumza kuhusu ujenzi wa wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza na kutoa shukurani kwa wadau wote ikiwemo Shirika la JHPIEGO kwa kusaidia ujenzi wa wodi hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika- Prof. Mohamed Janabi, Viongozi wa Serikali na wadau wa maendeleo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Viongozi na wadau mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi akimpongeza mmoja wa akina mama katika wodi mpya ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Baadhi ya wazazi katika wodi ya watoto njiti iliyopo Hospitali ya Wilaya Kwimba mkoani Mwanza wakifurahia mazungumzo na viongozi wakati wa uzinduzi wa wodi hiyo.
Mwonekano wa miongoni mwa nyumba za watumishi zilizojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Kikundi cha Sungusungu Wilaya ya Kwimba kikitoa burudani ya asili wakati wa uzinduzi wa wodi ya watoto njiti iliyojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com