Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KISHAPU YADHIHIRISHA NGUVU YA UMOJA KILELE CHA TAMASHA LA AMANI NA MAENDELEO

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga na mgeni rasmi wa kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu lililoanza Februari 23 hadi 28,2026  Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humo

Na Sumai Salum-Kishapu

Kishapu imeandika historia mpya Kuanzia tarehe 23 hadi 28 Februari 2026, viwanja vya mpira vya Shule ya Msingi Buduhe Kata ya Kishapu vimekuwa kitovu cha mshikamano, furaha na uzalendo kupitia Tamasha la Amani na Maendeleo.


Akihutubia katika kilele cha tamasha hilo,Mbunge wa Jimbo la Kishapu na Mgeni rasmi, Mhe. Lucy Thomas Mayenga, amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika michezo na shughuli mbalimbali zilizolenga kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya wilaya.


“Nawapongeza sana wananchi wwnzangu wa Kishapu kwa kuonyesha upendo, mshikamano na ari ya maendeleo. Tamasha hili limeonyesha wazi kuwa tunapoungana, tunaweza kufanya mambo makubwa. Amani ni msingi wa maendeleo yetu, na michezo ni daraja la kuimarisha umoja wetu,” amesema Mhe. Mayenga kwa shangwe za wananchi.


Tamasha hilo lilipambwa na michezo na burudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili zilizotikisa jukwaa, mashindano ya kukamata kuku yaliyoibua vicheko na nderemo, kuvuta kamba kulikodhihirisha nguvu na ushirikiano, pamoja na michezo ya mpira wa pete, mpira wa nyavu na mpira wa miguu iliyoshirikisha vijana na watu wazima kwa pamoja.


Mhe. Mayenga pia aliwashukuru madiwani, wakuu wa taasisi, mashirika mbalimbali pamoja na viongozi wa Kata na Vijiji kwa ushirikiano wao mkubwa katika kufanikisha tamasha hilo. Amesisitiza kuwa mafanikio ya tamasha hilo ni matokeo ya mshikamano wa viongozi na wananchi kwa ujumla.Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga na mgeni rasmi wa kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu lililoanza Februari 23 hadi 28,2026  Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humo


“Maendeleo hayaji kwa mtu mmoja. Yanahitaji ushirikiano wetu sote viongozi wa serikali, taasisi, mashirika na wananchi. Leo mmeonyesha mfano bora wa namna Kishapu inaweza kusonga mbele,” ameongeza.


Mhe. Lucy ameongeza kuwa, matamasha kama hayo yana faida kubwa kwa maendeleo ya jamii, ikiwa ni pamoja na  kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi bila kujali tofauti zao za kijamii au kisiasa, yanatoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao katika michezo na sanaa, jambo linaloweza kuwa chanzo cha ajira na kipato na kuimarisha afya za wananchi kupitia ushiriki wa michezo mbalimbali, huchochea shughuli za kiuchumi kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kuuza bidhaa na huduma wakati wa tamasha.


Aidha, amewahimiza vijana kutumia vipaji vyao katika michezo na sanaa kama fursa ya kujiletea kipato na kujenga nidhamu, akiahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zote zinazolenga kukuza michezo na kuimarisha ustawi wa jamii.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na mwandaaji wa Tamasha la Amani na Maendeleo Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye kilele cha tamasha hilo lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humo


Mkuu wa Wilaya Hiyo Mhe. Peter Masindi amesema, michezo ni nyenzo muhimu si tu kwa burudani bali pia kwa ajira na maendeleo ya vijana. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayosaidia kuibua na kukuza vipaji vya vijana ili viweze kuwainua kiuchumi.


“Michezo ni ajira. Vijana wetu wana vipaji vikubwa vinavyohitaji kuendelezwa. Matamasha kama haya ni sehemu ya mkakati wa kuwawezesha vijana kujitegemea na kuchangia maendeleo ya Wilaya ya Kishapu,” amesema Mhe. Masindi.Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na Fatma Mohamed akizungumza kwenye kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo  lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humo


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri Josephat Limbe, ameeleza kuwa michezo ni sekta inayokua kwa kasi na inaweza kuwa chanzo kikubwa cha ajira endapo itawekewa mikakati madhubuti na kuungwa mkono na wadau mbalimbali. Aliahidi kuwa Halmashauri itaendelea kuboresha miundombinu ya michezo na kuandaa mashindano mara kwa mara ili kuwapa vijana fursa zaidiMwenyekiti wa Halmashauri ya wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Josephat Limbe, akiwa kwenye kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo  lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humo


Baadhi ya Wananchi walioshiriki tamasha hilo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ya uongozi wa wilaya. Pili Mazoya amesema tamasha hilo limeimarisha mshikamano na kuleta furaha kwa jamii.


“Tunampongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuandaa tamasha hili. Limekuwa fursa ya kukutana, kuimarisha umoja na kuhamasisha vipaji vya vijana,” amesema Sophia.


Naye Jitili Deus Kasekwa amesema matukio kama hayo yanapaswa kuendelea kufanyika mara kwa mara kwani yanaongeza motisha kwa vijana na kuimarisha uchumi wa wananchi.


“Si burudani tu, bali ni fursa ya ajira na maendeleo. Tunashukuru uongozi kwa kutuunganisha na kutuletea tamasha hili,” amesema KasekwaKaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Severine Msyangi, akiwa kwenye kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo  lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humo


Sambamba na hayo fainali iliyopigwa leo mchezo wa mpira wa miguu kungo namba 10 Anthonu Jacobo ameifanya Kishapy Veterani kuwa mshindi w akwanza wakifuatiwa na Kishapu Sekondari, mpira wa pete mshindi ni timu y Watumishi wakifuatiwa na Mwataga Sekondari na mshindi wa tatu kuwa ni isoso Sekondari na Mchezo wa Wavu  mshindi wa kwanza ni Watumishi veterani wakifuatiwa na Watumishi Kishapu na washindi wote wamepewa zawadi.


Kwa ujumla, Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu 2026 limeacha alama ya matumaini na mshikamano, likidhihirisha kuwa kwa umoja, amani na ushirikiano wa viongozi na wananchi, Kishapu inaendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Shija Ntelezu, akiwa kwenye kilele cha Tamasha la Amani na Maendeleo  lililoanza Februari 23 hadi 28,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani humoMkazi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Pili Mazoya, akizungumzia tamasha hilo Februari 28,2026Mkazi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Jitili Deus Kasekwa akizungumzia Tamasha hilo Februari 28,2026

























































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com