TMFD YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUWEKA MIKAKATI YA UVUVI ENDELEVU

Na Mwandishi wetu - Dar es Salaam

Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries  Development (TMFD) limekutana na wadau wa kimaendeleo na kufanya majadiliano mafupi ya namna ya kutumia vyombo vya habari kwenye kuhamasisha uvuvi endelevu Nchini.


Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko amekutana na wadau hao Jijini Dar es salaam na kuitambulisha TMF na kazi zake kwenye eneo la uvuvi na vyombo vya habari.


Soko amekutana na Naibu  Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bwana Kjetil Schie na kujadili fursa za kutumia vyombo vya habari kwenye kuhamasisha uvuvi endelevu.

Bwana Schie amesema kuwa anafurahishwa sana na uwepo wa TMFD kwenye eneo la uvuvi kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuhamasisha  uvuvi endelevu kwa kutumia vyombo vya habari


Pia mkurugenzi wa TMF mekutana na kufanya mazungumzo na  Mwakilishi Mkazi wa shirika la maendeleo la kimataifa la JICA Bibi Murao Akari juu ya umuhimu wa kuendeleza uvuvi kwa kutumia njia bora.


Bwana Soko amesema kuwa kwa sasa TMFD inajikita kwenye kupanua uwigo wa wadau ili kufanya kazi kwa pamoja kwa nia ya kuendeleza uvuvi endelevu Nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments