JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI YATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA BROTHER OF CHARITY

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde -Malunde 1 blog
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imetoa msaada Chakula kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na akili wanaolelewa katika Kituo cha Brothers of Charity kilichopo mtaa wa Majengo Mapya kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo leo Ijumaa Mei 12,2023, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko amesema CCM inatambua makundi ya watu wenye uhitaji ndiyo maana imewatembelea watoto hao na kuwapatia msaada.

“Tupo kwenye ziara ya kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini kutembelea kata mbalimbali kwa ajili kukagua uhai wa Jumuiya, kuingiza wanachama wapya na kuhamasisha kuanzisha miradi ya kiuchumi na tumekuja hapa kuwatembelea watoto wetu na kuwapatia hiki kidogo tulichokuja nacho na tunaahidi kuendelea kufika hapa na tunaomba wadau wengine na wananchi wajitokeze kusaidia watoto hawa”,amesema Mrindoko.

“Tunawashukuru walezi wa watoto hawa. Hii kazi mnayofanya kulea na kuwafundisha watoto hawa mambo mbalimbali kwakweli kazi hii mnayofanya ni kazi ya kitume. Tunawashukuru na tunawapongeza sana. Nimeambiwa watoto hawa walikuwa hawajui chochote lakini mmewafundisha jinsi ya kujitambua na sasa wanafanya wao wenyewe. Asanteni sana nasi tunaendelea kukitangaza kituo hiki lakini pia tutaendelea kufika hapa ili tushirikiane kutatua changamoto zinazojitokeza”,amesema.Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi amesema Jumuiya hiyo ina jukumu la malezi ndiyo maana watembelea kituo hicho cha watoto na kuwapatia chakula ikiwemo unga wa sembe, mchele, mafuta ya kupikia, chumvi, juisi na biskuti.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother George Paul Rice amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutembelea kituo hicho ambacho sasa kina watoto zaidi ya 20 na kuwapatia msaada wa chakula.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko  akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko  akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 12,2023.

Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother George Paul Rice wakati Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini ikitembelea kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Brother of Charity, Brother Francis Bega wakati Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini ikitembelea kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Sehemu ya chakula kilichotolewa na Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali wakikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kukabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga likiendelea

Muonekano bango katika kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments