MCHUNGAJI AKAMATWA SAKATA LA WAUMINI 98 KUFA KWA NJAA ILI WAMUONE YESU


Mchungaji wa Kanisa la New Life International Church, Ezekiel Odero lililopo kwenye eneo la Mavueni katika Kaunti ya Kilifi nchini Kenya amekamatwa.

Kukamatwa kwake kumekuja siku moja baada ya kuhojiwa kuhusu madai ya kuwa na uhusiano na Paul Mackenzie ambaye kanisa lake limesababisha vifo vya takriban watu 98 kwa kuwataka waumini wake wasile chakula ili wafe wakamuone Yesu.

Akithibitisha hilo Kamishna wa Mkoa wa Pwani Rhoda Onyanja amesema Ezekiel amekamatwa kufuatia madai ya vifo ambavyo vimekuwa vikitokea pia katika kanisa lake.

Onyanja amesema Kanisa la Ezekiel pia limefungwa kwa muda usiojulikana

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post