CHALAMILA : RPC KAGERA JIPANGE KWELI KWELI KUONDOA MAUAJI

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila amemtaka Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa kujipanga kikamilifu katika kutokomeza mauaji yanayoendelea katika Mkoa wa Kagera.


Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa na wananchi uliofanyika katika uwanja wa Mayunga uliopo mtaa wa Uswahilini Kata Bilele Manispaa ya Bukoba.

"Kumekuwepo mauaji sasa RPC jipange. Ninaposema jipange ujipange kweli, Mimi sijawahi kushindwa na mtu anayejiita jambazi hata siku moja", amesema Mh. Chalamila.

Ameongeza kuwa Mkuu wa Mkoa anatakiwa kuhakikisha anakuwa mlinzi wa watu na mali na uhai wao na kwamba atasimama na Polisi kuhakikisha hali ya Mkoa inakuwa shwari.


Sambamba na hayo amewataka Polisi wanaofanya doria majini na kuchukua fedha pamoja na kunyang'anya injini za wavuvi na kuziuza kuacha mara moja.


"Kama kuna askali mla rushwa au kiongozi na mtu yeyote ndani ya ofisi yangu mla rushwa akajipange vizuri kwamba aliekuja atakuchoma na moto wa hapa duniani" amesema Mh. Chalamila.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post