Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

GIZA DARAJA LA MHUMBU LAWATISHA WANANCHI BUGWETO, WATAKA TAA ZA BARABARA YA MWANZA–SHINYANGA ZIWASHWE

Na Kadama Malunde _ Malunde 1 blog

Wananchi wa eneo la Bugweto katika Manispaa ya Shinyanga wameiomba mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuwasha taa za sola zilizowekwa kando ya barabara ya Mwanza–Shinyanga ambazo kwa sasa hazifanyi kazi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kutofanya kazi kwa taa hizo kumesababisha giza kubwa hasa nyakati za usiku, hali inayohatarisha usalama wa watembea kwa miguu pamoja na watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Wameeleza kuwa maeneo hatarishi zaidi ni kuanzia kona ya Bugweto hadi katika eneo la sheli, pamoja na eneo la daraja la Mhumbu, ambako giza ni kubwa na linaweza kusababisha ajali au matukio ya uhalifu.

“Tunaiomba mamlaka husika zifike hapa haraka kukagua taa hizi za sola ili zirekebishwe na kuwashwa upya. Giza ni kubwa sana hasa katika eneo la daraja la Mhumbu na linaweka maisha ya watu hatarini. Tayari vibaka wanazungukia eneo hili, wapo kazini,” 
amesema mmoja wa wananchi wa eneo hilo aliyenusurika kukabwa na vibaka.

Wananchi hao wamesema taa za barabarani zina umuhimu mkubwa katika kuimarisha usalama wa jamii pamoja na kusaidia kudhibiti ajali na vitendo vya uhalifu, hivyo wameomba mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kurekebisha taa hizo.

Aidha, wameiomba Manispaa ya Shinyanga pamoja na mamlaka zinazohusika na miundombinu ya barabara kuhakikisha taa hizo zinakarabatiwa au kubadilishwa ili ziweze kuwaka tena na kuendelea kuhudumia wananchi.

Tazama Video

@malundeblog

 WANANCHI BUGWETO SHINYANGA WAOMBA TAA ZA SOLAR BARABARA YA MWANZA–SHINYANGA ZIWASHWE Wananchi wa eneo la Bugweto katika Manispaa ya Shinyanga wameiomba mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuwasha taa za sola zilizowekwa kando ya barabara ya Mwanza–Shinyanga ambazo kwa sasa hazifanyi kazi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kutofanya kazi kwa taa hizo kumesababisha giza kubwa hususan nyakati za usiku, hali inayohatarisha usalama wa watembea kwa miguu pamoja na watumiaji wengine wa barabara. Wameeleza kuwa maeneo hatarishi zaidi ni kuanzia kona ya Bugweto hadi katika eneo la sheli, pamoja na eneo la daraja la Mhumbu, ambapo giza ni kubwa na linaweza kusababisha ajali au matukio ya uhalifu. “Tunaiomba mamlaka husika zifike hapa haraka kukagua taa hizi za sola ili zirekebishwe na kuwashwa upya. Giza ni kubwa sana hasa eneo la daraja la Mhumbu na linaweka maisha ya watu hatarini,” amesema mmoja wa wananchi wa eneo hilo. Wananchi hao wamesema taa za barabarani ni muhimu kwa usalama wa jamii na kusaidia kudhibiti ajali pamoja na vitendo vya uhalifu, hivyo wameomba hatua zichukuliwe mapema ili kurejesha hali ya usalama katika eneo hilo. Aidha, wameiomba Manispaa ya Shinyanga pamoja na mamlaka zinazohusika na miundombinu ya barabara kuhakikisha taa hizo zinakarabatiwa au kubadilishwa ili ziweze kuwaka tena na kuendelea kuhudumia wananchi.

♬ original sound - Malunde





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com