RC CHALAMILA AMUAGIZA RPC KAGERA KUPUNGUZA VIZUIZI MTUKULA MPAKA BUKOBA

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila amemtaka Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera ACP William Mwampaghale kupunguza vizuizi (beria) zilizopo Mtukula mpaka Bukoba.

Akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa na wananchi uliofanyika katika uwanja wa Mayunga uliopo mtaa wa Uswahilini Kata Bilele Manispaa ya Bukoba amesema kumekuwa na vizuizi vingi katika barabara la kutoka Mtukula mpaka Bukoba ambavyo vimekuwa vya kuonea wannchi na kuwatoa rushwa.


Ameongeza kuwa vizuizi hivyo vimekuwa vikiwekwa kwa ajili ya rushwa na kunyang'anya mali za wananchi jambo ambalo sio zuri na ni kosa kisheria.


"Kagera anayoitaka Mhe. Rais Samia ni ya wananchi kuwa huru na biashara zao na sio kutengeneza vizuizi ambavyo wengine ni wala rushwa na kunyang'anya mali za masikini", amesema Mhe. Chalamila.

Ameongeza kuwa jukumu moja wapo alilotumwa na Mh. Rais Samia ni kutotaka kusikia kilio kwa wananchi wake anaowaongoza.


"Na hili ni agizo la kwanza kwa RPC kukaa na vyombo vingine kutoa maberia mengine yasiyo na msingi kutoka kule Mtukula, Kyaka mpaka kufikia Rwamishenye kumejaa maberia matupu lakini mwisho wa siku mfanyabiashara mdogo ananyang'anywa mali zake", amesema Mhe. Chalamila.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post