MPIGA DEBE AFARIKI KWA KUKANYAGWA GARI AKIFUKUZIA POSHO YAKE KWENYE BASI


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mpiga debe mmoja wa eneo la Makambako mkoani Njombe amefariki dunia kwa kukanyagwa na gari katika kichwa chake kutokana na kuanguka wakati akifukuzia basi linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kupata posho yake ya kupakia abiria.


Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibitisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

“Mpiga debe alikuwa amefuata fedha yake kwa ajili ya abiria aliokuwa amewapakia na kwa bahati mbaya ule mlango wakati unajifunga aliweza kusukumwa na akadondokea kwenye uvungu na tairi za nyuma za gari ziliweza kumpitia,” alisema Kamanda Issah.

Ametoa wito kwa wafanyakazi wa maeneo ya stendi kuwa makini na kuangalia usalama wao wakati wa kufanya kazi zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments