MATOKEO YA MTIHANI WA 23 WA KITAALUMA WA UNUNUZI NA UGAVI YATANGAZWA


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi Godfred Mbanyi akiongea na Waandishi wa habari leo Dodoma (hawapo pichani) kuhusu matokeo ya mtihani wa 23 wa kitaaluma kuhusu ununuzi na ugavi huku akieleza kuwa wanafunzi wengi hufeli masomo yanayohusu mahesabu jambo wanalotaka kulitilia mkazo kuona nini cha kufanya.

*****

Na Dotto Kwilasa, Malunde1 blog-DODOMA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)  Godfred  Mbanyi ametangaza matokeo ya mtihani wa 23 ya kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi kuwa jumla ya Wadahiliwa walikuwa 479,kati yao waliofanikiwa kufanya mitihani ni 427 ambapo 28 kati yao hawakufanya kabisa mtihani huo.

Pamoja na hayo Godfred Mbanyi amesema kuwa wanafunzi 65 wamefeli kabisa ambapo ni sawa na asilimia kumi na nne 14.4%  hivyo wanatakiwa kurudia mitihani hiyo katika ngazi ambazo walirisiti kufanya mitihani hiyo huku akielezea kuwa kila ngazi inakuwa na mitihani minne hivyo hawa waliofeli wanapaswa kurudia mitihani yote.

Akiongea na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma,amesema watahiniwa 230 wanatakiwa kurudia baadhi ya mitihani waliyofeli  (Suplimentary) ili kukidhi ufaulu katika masomo ambayo hawakufanya vizuri.

"Katika mitihani mingi ya Bodi inayohusiha maswala ya mahesabu ,takwimu, Uchumi na masomo mengine yenye kuhusisha hesabu wanafunzi wamekuwa wakifanya vibaya pia mitihani ya kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi kuna wanafunzi pia wamefeli hivyo wanapaswa kufanyia kazi kwa sababu ndio maeneo ambayo watakwenda kufanyia kazi,"amesema

Pamoja na hayo amefafanua kuwa jumla ya Masomo ni 32 huku akisema kati ya hayo Masomo 6 wamefanya vibaya sana ,17 ni ufaulu wa Wastani na masomo 11 wamefanya vizuri kiasi  na kufanya jumla ya wastani wa ufaulu katika mitihani hiyo ya Bodi ya kataalamu ya Ununuzi na Ugavi kuwa ni asilimia 34.6% kwa mitihani hii ya 23.

"Niwatake wanafunzi wote waliofeli mitihani na wale wanaotakiwa kurudia kuhakikisha wanajisajili tena kwa ajili ya kufanya mitini hiyo,natangaza rasmi kuwa kwanzia Jumatatu ya tarehe 14 ,Machi 2022 dirisha litakuwa wazi kwa ajili ya wanafunzi watakaohitaji kufanya mitihani hii ya bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ;

Fomu za kujiunga zitapatikana katika tovuti ya bodi hivyo usajili wote utafanyikia mtandaoni (Online) na kuwataka wanafunzi kujiyokeza kwa wingi kuomba nafasi hiyo ya kufanya mitihani ya Kitaaluma ya ununuzi na ugavi,"amesisitiza.

Katika hatua nyingine,Mkurugenzi Mtendaji huyo wa PSPTB ameeleza kuwa kuna haja ya wao kutembelea Vyuo mbalimbali pamoja na shule za sekondari nchini ili kubaini tatizo linalochangia wanafunzi wengi kufeli masomo ya sayansi.

Amesema,hali hiyo itaibua hoja na hamasa ya wanafunzi wengi kuchangamkia fursa ya masomo hayo na kuzalisha wasomi wengi wa masuala ya ununuzi na ugavi kwa uchumi wa viwanda.

"Katika mitihani inayofanywa wengi hufeli kwenye masomo ya hesabu kutokana na hali hii tumejipanga kutembelea Vyuo mbalimbali nchini kuona tatizo linaanzia wapi na nini kifanyike kuondoa tatizo hili,"amefafanua Mkurugenzi Mkuu huyo wa PSPTB.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post