NSSF YAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA KUKUZA USHIRIKIANO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil mjini Unguja. Mara baada ya kuhutubia Mhe. Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi alifungua rasmi mkutano huo. Mkutano huo umedhaminiwa na taasisi mbalimbali ikiwemo NSSF ambayo ilipata fursa ya kutoa semina kwa wahariri kuhusu hifadhi ya jamii, majukumu na Utendaji wa Mfuko


Na MWANDISHI WETU

Ni historia nyingine muhimu iliyoandikwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) baada ya kukutana na wadau wake ambao ni Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kuwapa semina kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na Mfuko katika kuijenga na kustawisha sekta ya hifadhi ya jamii nchini pamoja na kueleza dhamira yake ya kukuza maendeleo endelevu ya Taifa.


Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil mjini Zanzibar baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa jukwaa hilo uliokuwa na kauli mbiu isemayo "Uchumi wa Buluu na Mawasiliano ya Umma".


Akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba alisema kupitia mkutano huo Mfuko ulitoa semina kuhusu majukumu ya msingi ya Mfuko ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta rasmi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.


Mshomba alisema Mfuko unaunga mkono jitihada mbalimbi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi makini wa Rais Dkt. Mwinyi hasa katika kutimiza dhana na muelekeo ya Serikali kupitia uchumi wa buluu.


Mshomba alisema Mfuko umedhamini mkutano huo kwa kutambua umuhimu wa jukwaa hilo hasa ukizingatia kuwa ulitumia mkutano huo kuwajengea uelewa wahariri hao wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa maisha ya sasa na baadaye.


Alisema Mfuko umevutiwa zaidi na ushirikiano mzuri uliopo na wadau wake wakiwemo wanahabari na kwamba ushirikiano huo utaendelea kuwa endelevu.


Akitoa mada kuhusu shughuli zinazofanywa na Mfuko, Meneja Usimamizi Mafao wa NSSF, James Oigo aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo dhana ya hifadhi ya jamii, majukumu, muundo panoja na NSSF.


Oigo pia aliwapitisha kwa kina wahariri hao kufahamu majukumu manne ya Mfuko na kueleza namna ambavyo Mfuko umezidi kusogeza huduma zake karibu na wanachama kupitia mifumo ya Tehama.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alipongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Mfuko hasa katika kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa Watanzania waliojiajiri kupitia sekta rasmi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, mama lishe, bodaboda na wajasiriamali wengine.


Alisema NSSF inafanyak azi kubwa na nzuri inayoonekana kwa kuunga mkono
juhudi mbalimbali za Serikali ikiwemo Serikali ya Zanzibar katika kutimiza dhana yake ya uchumi wa buluu.


Naye Mhariri wa habari mwandamizi ambaye pia ni mjumbe wa TEF, Bakari Kimwanga aliipongeza NSSF kwa kudhamini mkutano huo ambao umetoa fursa ya kuweza kufahamu mambo mbalimbali yakiwemo ya hifadhi ya jamii pamoja na sera ya Serikali ya Zanzibar ya uchumi wa buluu.


Awali, Mhariri mwanamizi, Jesse Kwayu aliwataka Watanzania hasa walioajiriwa katika sekta rasmi kuondoa fikra za kutaka kuchukua fedha zao mapema kwani wakifanya hivyo watapata tabu watakapofikia uzeeni.


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kupitia mkutano huo NSSF ni mdhamini mkuu.
Meneja Usimamizi Mafao kutoka NSSF James Oigo akitoa mada kuhusu shughuli zinazofanywa na Mfuko wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambapo NSSF ndio mdhamini mkuu wa mkutano huo
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Iddrisa Kitwana Mustafa akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa jukwaa la wahariri Tanzania uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wahariri wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania uliofanyika Zanzibar
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akiongea na wahariri na kushukuru Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuwa mdhamini Mkuu wa mkutano wa mwaka wa jukwaa la wahariri Tanzania uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita, akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Balozi Ali Iddi Siwa cheti cha shukrani kwa Mfuko huo kudhamini Mkutano Mkuu wa TEF.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na viongozi waliokuwa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania wakiuliza maswali na kutoa Maoni baada ya NSSF kuwasilisha mada katika mkutano huo
Baadhi ya viongozi na maafisa kutoka NSSF wakijibu maswali na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari baada ya semina kwa wahariri. Jukwaa la Wahariri waliandaa mkutano wao wa mwaka uliofanyika Zanzibar. NSSF ni mojawapo ya wadhamini wa mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments