WATUPWA JELA KWA KUMUUA KWA KUMPIGA KIGODA ALIYEMIMINA POMBE YAO


Picha ya mfano wa mtu anayemimina pombe ya kienyeji
**

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma imewahukumu jela miaka miwili, watu wawili Tumaini Thomas na Jonas Mbilimi, wakazi wa Nyachenda wilayani Kasulu baada ya kumuua mwenzao aliyemimina pombe yao ya kienyeji aina ya Wanzuki wakiwa wanalewa kwenye kilabu cha Pombe.

Kesi ya mauaji ya bila kukusudia namba 14 ya mwaka 2021 Jamuhuri dhidi yao ikisikilizwa na jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Lameck Mlacha, mnamo Septemba 5, 2020 washtakiwa wakiwa wanakunywa pombe marehemu akanyanyuka na kumimina pombe hiyo hali iliyosababisha ugomvi na marehemu alikimbia wakamuangusha na kumkanyaga na miguu pamoja na kumpiga na kigoda kichwani.

Upande wa Jamuhuri uliwasilisha ushahidi mashuhuda wa tukio hilo, Askari na ndugu pamoja na ushahidi wa daktari ulio eleza fuvu la kichwa upande wa kushoto lilivunjika na kifo kilisababishwa na kuvuja damu nyingi kwenye ubongo.

Upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Joseph Mathias washtakiwa walisema walikuwepo wakati wa tukio na ugomvi ulivyoibuka mmoja wao aliamua ili wasigombane kisha wakaenda nyumbani na baadae kupata taarifa ya kifo hicho.

Jaji Mlacha baada ya kuangalia ushahidi wa pande zote amesema washtakiwa wameidanganya mahakama kwa kuwa mashahidi walio kuwepo walishuhudia tukio pamoja na maelezo ya marehemu kwa familia kabla hajafa hivyo ikawakuta na hatia ya mauaji ya bila kukusudia na wakili wa Jamuhuri Benedict Kivuma akaomba adhabu kali.

Via EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments