BERNARD MEMBE ASAMEHEWA, ARUDISHIWA UANACHAMA CCM - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Thursday, March 31, 2022

BERNARD MEMBE ASAMEHEWA, ARUDISHIWA UANACHAMA CCM


Bernard Membe akiwa kwenye moja ya kazi za CCM
*
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Taifa kilichofanyika leo Machi 31, 2022 Jijini Dodoma, kimeamua kumrejeshea kadi mwanachama wake Bernard Membe ambaye alifutiwa uanachama.

Membe pamoja na wanachama wengine waliorejeshewa kadi zao watakabidhiwa kwenye maeneo waliyopo.

Membe ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwenye serikali ya awamu ya nne, alifukuzwa uanachama wa CCM Februari 28, 2020 kufuatia uamuzi ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Taifa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages