KINANA KUMRITHI MANGULA - CCM...UCHAGUZI KUFANYIKA KESHO

 

Abdulrahman Kinana

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM) kimempendekeza Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama hicho Abdulrahman Kinana  kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho baada ya aliyekuwa mwenyekiti  Philip Mangula  kuwasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia ngazi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 31, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka imeeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa akishik nafasi hiyo Philip Mangula  kuwasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia ngazi.

Amesema Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea Barua rasmi ya kujiuzulu kwenye nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mzee Phillip Mangula.

 "Mangula amemwandikia Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo amewasilisha mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Kwaajili ya kukidhi matakwa ya kikanuni na Kikatiba


Ndugu Phillip Japhet Mangula amefikia uamuzi huo ili kukidhi Matakwa ya Kikatiba Ibara ya 9, kifungu kidogo(e) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la mwaka 2022, pamoja na Kanuni ya 116(e) ya kanuni ya Uchaguzi ya CCM Toleo la Mwaka 2017”,amefafanua.

Shaka amefafanua kuwa kwa Vifungu hivyo vya Kikatiba na baada ya Halmashauri Kuu ya CCM Kupokea na kuridhia Barua hiyo, hivyo Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imebaki wazi

“Na katika kukidhi matakwa ya kikanuni Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi atachaguliwa katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kupokea Ombi hilo wamefanya uteuzi wa mwanachama wa CCM ambaye atapelekwa kwenye Mkutano Mkuu kwaajili ya Kugombea nafasi ya Makamu Mwennyekiti wa CCM, Tanzania Bara”,amesema.

Amesisitiza kuwa hayo yamefanyika ili kukidhi matakwa ya Kikatiba Hivyo Halmashauri Kuu imemteua Ndugu, Abdulrahman Kinana ambaye ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kuwa Mgombea wa Umakamu Mwenyekiti wa chama hicho.

“Uchaguzi wake utafanyika kesho(April 01 kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi”,amesema.

CCM imemshukuru Ndugu Phillip Mangulla kwa Utumishi wake uliotukuka ndani ya Chama cha Mapinduzi ambaye amefanya kazi ndani ya Chama kuanzia Mwaka 2012-2022.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments