Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WA MAJI NCHINI WAKUTANA KUBORESHA USHIRIKIANO

Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog- DOODMA

KUELEKEA wiki ya maji,Wizara ya maji imefanya Mkutano wa wadau wanaotekeleza miradi ya maji ili kushauri na kutoa mapendekezo ya kuboresha ushirikiano baina ya Wizara na wadau utakao ongeza kasi ya ujenzi wa miradi ya maji na masuala yanayohusiana na sekta hiyo nchini.

Baadhi ya wadau hao ni wakandarasi,wahandisi washauri,wamiliki wa viwanda vinavyozalisha vifaa vya ujenzi wa miradi ya maji ,wasambazaji wa vifaa vya ujenzi wa miradi ya maji ,wasambazaji wa madawa ya kutibu maji na makampuni ya utafiti na uchimbaji wa visima.

Akiongea kwenye Mkutano huo leo Machi 10,2022 Jijini Dodoma,Waziri wa maji Juma Aweso amesema Mkutano huo ni muhimu kwa kuwa umebeba maudhui ya kuboresha ushirikiano baina ya Wizara na wadau hao hali itakayosaidia miradi ya maji Nchini kutekelezwa kwa uwazi na uwajibikaji .

"Tujenge utaratibu wa kuzungumza na wakandarasi Kila mwaka,hii itasaidia kuibua changamoto nyingi ambazo zitapata nafasi ya kutatuliwa na hatimaye kuondokana kabisa na uhaba wa maji,"amesema.

Hata hivyo Waziri huyo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri kupanga muda wa kusikiliza malalamiko ya wadau wa maji ikiwemo Yale yanayohusu kucheleweshewa malipo yao ili kuweka usawa kwenye sekta hiyo.

"Kumekuwa na malalamiko mengi kuwahusu wakurugenzi wa baadhi ya Halmashauri,yani kumpata Waziri au Katibu Mkuu ni rahisi mno kuliko kuwapata wao,niwaambie Kwa hai hii hatutaendana lazima tulikemee hili na kama hamtaki kubadilika tutawabadilisha kwa lazima,"amesema.

Sambamba na hilo Waziri Aweso amewata wasambazaji wa vifaa vya ujenzi wa miradi ya maji kuacha unyonge na kuhofia kutosikilizwa na Serikali na badala yake wahakikishe wanafuata ngazi huhisika za uongozi kabla ya kupeleka tenda.

"Wadau wetu msiwe wanyonge,msikubali kunyonywa ,hii wizara ina ngazi nyingi za ungo,hakikisheni tenda zote mnazopata zinapitia kwa wahusika ili kuondoa mkanganyiko uliopo,acheni kufuatia njia za panya zinawaponza mnakosa haki yenu,"amesisitiza Aweso.

Aweso pia amewataka wadau hao kuwa na umoja wao unao watamblisha ili wasidharaulike hali itakayowapa nafasi ya kuonyana wenyewe kwa wenyewe na hatimaye kuboresha taswirwa yao.

"Naamini pamoja na mapungufu yaliyopo bado kuna wakandarasi wazuri, Wizara ya maji hatuwezi kufanya kazi zote sisi wenyewe lazima tushirikiane na wadau wengine kufikia malengo ,tukiwa watendaji wazuri na kukamilisha miradi Kwa wakati na ushirikiano usio na hofu ni rahisi kuaminika,"amesema.


Nao baadhi ya wadau wa sekta ya maji wameeleza changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wao kuwa wamekuwa wakisumbuliwa wanapofuatilia malipo yao hivyo kuiomba Serikali kupitia wizara hiyo kuona haja ya kufuatilia suala hilo ili walipwe kwa wakati na kujiendeleza kiuchumi.

Akiongea mwa niaba ya wengine,mmoja wa wadau hao Isabella Mapunda kutoka Kampuni ya Mama Mapunda General Supply amesema wakandarasi wengi wanaotekeleza miradi ya maji sio waaminifu kwani wanakwamisha juhudi za wadau Katika kutatua kero ya maji.

"Tunadharauliwa, tunapeleka vifaa lakini hatulipwi kwa wakati ,tunazungushwa sana,tunapoanza kufatilia malipo yetu wanatujibu kuwa malipo yetu bado hayajakailika,wakati wahusika Wakuu wanateleza kuwa tayari fedha imeingia,"amesema
Baadhi ya wadau wanaotekeleza miradi ya maji wakiwa kwenye mkutano wa maji jijini Dodoma wenye lengo la 
kushauri na kutoa mapendekezo ya kuboresha ushirikiano baina ya Wizara na wadau hao utakao ongeza kasi ya ujenzi wa miradi ya maji na masuala yanayohusiana na sekta hiyo nchini .
Waziri wa Maji Juma Aweso akiongea kwénye Mkutano wa wadau wa Maji leo jijini Dodoma na kutumia nafasi hiyo kuwata wasambazaji wa vifaa vya ujenzi wa miradi ya maji kuacha unyonge na kuhofia kutosikilizwa na Serikali na badala yake wahakikishe wanafuata ngazi husika za uongozi kabla ya kupeleka tenda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com