AFARIKI BAADA YA KUPIGWA PEMBE LA NG'OMBE AKIPIGANA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, December 14, 2021

AFARIKI BAADA YA KUPIGWA PEMBE LA NG'OMBE AKIPIGANAMWANAUME mmoja mwenye umri wa miaka 40, Joseph Weremba kutoka Kijiji cha Mtetemo, eneo Bunge la Mumias Mashariki, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya aefariki dunia baada ya alipigwa pembe la ng’ombe wake dume aliyemnunua wiki iliyopita wakati ng’ombe wake akipigana na ng’ombe mwingine wa kaka yake.


Taarifa iliyotolewa na baba mzazi wa wa Joseph, Jared Weremba amesema Joseph alimnunua fahari huyo wiki moja iliyopita na alikuwa akifanya mazoezi akijiandaa kwa pigano ambalo lingefanyika Disemba 26.


Walioshuhudia kisa hicho, walidokeza kwamba fahali wa Joseph alizidiwa nguvu kwenye pigano hilo, na kumgeukia bosi wake kisha kumpiga pembe kifuani kabla ya kumrusha upande wa nyuma. Mwendazake alivuja damu hadi kufa na mwili wake kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya St Mary’s Mumias.


Tambiko ambalo hufanywa wakati mikasa kama hiyo ikifanyika, liliandaliwa na fahali huyo kukatwa vipande vipande. Tambiko hilo linasemakana kuwa na umuhimu wa kuwakinga wanafamilia dhidi ya mapepo ambayo yanaweza kujitokeza na kusababisha mkasa mwingine kama huo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages