DADA AMUUA KAKA YAKE WAKICHAPANA MAKONDE NYUMBANI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, November 30, 2021

DADA AMUUA KAKA YAKE WAKICHAPANA MAKONDE NYUMBANIMwanaume mwenye umri wa miaka 40 katika Kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya ameaga dunia baada ya kuzozana na dadaake nyumbani kwao mtaani Kwanza.

Daniel Kipketer na dadaake Jane Chebor, 48, waliripotiwa kukorofishana kuhusiana na jambo ambalo halijathibitishwa, kabla ya wawili hao kutandikana nyumbani kwao katika kijiji cha Soyimining "B".

 Kulingana na DCI Chebor alijihami kwa fimbo ambayo aliitumia kumpiga marehemu kakake kisogoni, na kukatisha maisha yake katika makabiliano hayo.

 "Marehemu hakuonekana kuwa na jeraha lolote kichwani baada ya tukio hilo lakini alianza kutokwa na damu puani na hatimaye akaanguka chini kabla ya kuzimia na kufariki dunia," DCI alisema.

 Wapelelezi huko Trans Nzoia walimkamata Chebor na silaha iliyotumiwa kumpiga marehemu ilipatikana katika eneo la tukio.

Mwili wa marehemu unasubiri kufanyiwa upasuaji katika makafani ya Hospitali ya Rufaa ya Kitale. 

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages