MWAMBA ALIYEKUWA ANAUZA SENENE KWENYE NDEGE AKAMATWA



Mwanaume anayeshutumiwa kwa kuuza panzi(senene) waliokaangwa kwa wasafiri waliokuwa ndani ya ndege ya Uganda- Ugandan Airlines ameshitakiwa na polisi pamoja na mwanaume mwingine ambaye anashutumiwa kwa kuchukua video ya tukio hilo.

Mubiru Paul na Hajib Kiggundu walikamatwa Jumatatu walipowasili na kushitakiwa mashitaka matatu – kusababisha kero, kukataa kufuata maagizo ya wahudumu wa ndege na vitendo vya uzembe ambavyo vinaweza kusababisha kusambaa kwa maambukizi ya maradhi.

Shitaka la kusambaza maambukizi ya maradhi linaweza kusababisha kifungo cha miaka saba jela, limeripoti gazeti la Daily Monitor nchini humo.

Kampuni hiyo ya ndege ya Uganda ililaani kile ilichokiita tukio la "kuvuruga" utaratibu na vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa baadhi ya wafanyakazi wamesimamishwa kazi.

Uganda Airlines ilisema itaangalia uwezekano wa kuongeza mlo wa nsenene kwenye menyu yake kwa wasafiri watakaoomba, baada ya kubaini kuwa msisimuko wa wasafiri waliokuwemo ndani ya ndege walipoona nsenene ulitokana na uhaba wa idadi ya panzi hao msimu huu.

Picha za video za tukio hilo zilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii tangu tukio hilo lilipotokea mwishoni mwa juma:

Social embed from twitter


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments