KOCHA GOMES : NIMEAMUA KUJIUZULU NAFASI YANGU YA UKOCHA WA SIMBA ...


Ikiwa ni saa chache baada ya kutangazwa kuachana na Klabu yake yake, aliyekuwa Kocha wa Simba, Didier Gomes Da Rosa raia wa Ufaransa, amezungumza na wanahabari baada ya Simba kutangaza rasmi kuwa wameachana nae leo Oktoba 26, 2021.

“Ninapenda kuwa muwazi kwa mashabiki na wapenzi wa mpira nchini Tanzania, nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ukocha Mkuu wa Simba Sc kwa sababu ninaamini ndiyo maamuzi sahihi kwa manufaa ya klabu.

“Baada ya mechi ile tulikuwa kwenye wakati mgumu, disappointment ni kubwa sana, huzuni ni kubwa, mimi kama kocha mkuu nina wajibu wa kuwajibika kwenye hili, ndiyo maana nikachukua maamuzi ya kujiuzulu. Siwezi kulaumu chochote wala kumlaumu yeyote, ninaipenda Simba Sc, ninamtakia kila la kheri kocha mpya.

“Ninawashukuru sana mashabiki wa Simba kwa sapoti yao, wamekuwa na mimi kila siku. Ninamshukuru kocha wangu msaidizi, tumefanya kazi kubwa katika kipindi chote ambacho tumekuwa wote Simba, kocha wangu wa makipa naye amefanya kazi kubwa sana.

“Mwanzo wa msimu tumeanza na wachezaji wengi wapya, wachezaji wetu wawili wameondoka (Miquissone na Chama), ni jambo gumu kidogo. Lakini kama ambavyo nimekuwa nikisema, kwa kikosi hiki cha Simba, kinaweza kufanya makubwa na kufika mbali.

“Kilichotokea binafsi kimenihuzunisha na kimeweka doa kwenye carrier yangu ya ukocha, ni wakati wa kujipanga na kufanya makubwa zaidi. Kwa upande wa Simba ninaamini wakijipanga vizuri watashinda Ligi na Shirikisho.

“Kwanza namshukuru Mo Dewji kwa sababu ni mtu wa kutekeleza maneno yake, na nimekuwa naye karibu katika kila mikakati yangu ndani ya Simba. Hata muda mchache uliopita nimeongea nao kuwatakia kila la heri katika mashindano ya Shirikisho.

Kuhusu kujiunga na Yanga. “Kwa Ufaransa, Kocha wa PSG hawezi kuwa kocha wa Marseille, hata Hispania Kocha wa Barcelona hawezi kuwa kocha wa Madrid. Nimepokea ofa miezi mitatu iliyopita, nitaangalia na wakala wangu, siwezi kuongea sana kuhusu hayo leo,” amesema Kocha Didier Gomes Da Rosa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments