MREMBO ANAYESIFIKA KUTAPELI WANAUME BAADA YA KUHONDOMOLANA NAO AONJA JOTO YA MGANGA WA KIENYEJI


Mrembo aliyesifika mtaani Korogocho, Nairobi Kenya kwa ujanja wake wa kuwatapeli wanaume maelfu ya pesa baada ya kushiriki mahaba nao amebanwa asijue la kufanya baada ya kukutana ana kwa ana na mjanja wao.

Duru zinaarifu kwamba mrembo ambaye alikuwa akifanya kazi ya ukahaba alikuwa ametafuna pesa za wanaume kupindukia.

 “Kisu kimegusana na mfupa. Hapa kwangu utakula huu na hasara juu. Ondoka sasa ama niambie vijana wangu wakufanyie kazi,” mrembo alitishwa na jamaa aliyelenga kumpora ambaye ni Mganga wa Kienyeji.

Kwa mujibu wa Taifa leo, kila wakati mrembo huyo alipotembea na mwanaume alimtishia kwa kisu na kudai kulipwa pesa nyingi na kila mwanaume aliyekosa hela alipokonywa simu au chochote cha thamani ndani ya nyumba.

Hata hivyo, siku ya arobaini ya mrembo ilipofika alikutana na jamaa katika kilabu kimoja. 
Walibugia vileo na kisha lofa akaamua kumpeleka kwake. Walilishana uroda usiku kucha kisha alfajiri demu akadai alipwe KSh 5000 sawa na takribani shilingi laki Moja ya Tanzania.

 Jamaa alikuwa na KSh 500 (sawa na shilingi elfu 10 ya Tanzania) pekee mfukoni. “Nitoe wapi pesa hizo jamani? Nina KSh 500 tu,” jamaa alimpasulia mbarika dada huyo.

“Wewe leo utajua hujui! Unajua unacheza na nani wewe? Mimi huminya mwanaume akinipigia magoti na kunililia,” kisura alitisha akimrusia kofi lakini ilidakwa.

 “Leo umepatana na dume lisiloogopa visu wala bastola. Tazama humu kabatini. Waona nini?” jamaa alisema huku akimfungulia kabati mrembo. 

Mrembo alishangaa kuona mifupa mingi ya aina tofauti, jambo lililomtia woga usio wa kawaida. 

“Ukiendelea kunitishatisha, hutatoka katika nyumba hii. Nitahakikisha umekuwa chizi,” jamaa ambaye alikuwa mpiga ramli alimlukia dada huyo. 

Kisura aliondoka pole pole akafungua mlango na kutoweka bila kutazama nyumba. Aliapa kutokanyaga kwa jamaa tena akijua fika kuwa pwangu hupata pwaguzi.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments