Breaking

Post Top Ad

Wednesday, October 20, 2021

AVUNJWA MENO BAADA YA KUPUUZA ONYO LA 'KOJOA HAPA UONE'
Polisi mjini Kakamega nchini Kenya wamemkamata jamaa mmoja kwa kumpiga na kumjeruhi mwenzake aliyepuuza onyo kwa umma kutokojoa hadharani.

Katika kisa hicho, Jared Otieno,30, alikasirishwa baada ya mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 24, kupuuza onyo la “Kojoa Hapa Uone!” lililokuwa limeandikwa kwenye ukuta.

Katika taarifa kwenye Twitter siku ya Jumanne, Oktoba 19,2021 Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai( DCI) ilisema kuwa mwathiriwa hakuwa amemaliza kujisaidia wakati Otieno alitokea na kumpiga mangumi na mateke.

Mateke na mangumi ya Otieno yalivunja meno ya mwathiriwa na kuwacha uso wake ukiwa umevimba.

Mashahidi walijaribu kumtuliza Otieno aliyekuwa na hasira lakini walishindwa, huku akichukuwa sheria mkononi mwake na kuitiwa maafisa wa polisi kutka Kituo ca Polisi cha Kakamega.

Mwathiriwa ambaye alijeruhiwa vibaya, alishindwa kufungua mdomo wake sababu ya majeraha na kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Kakamega kwa matibabu.

Chanzo - Tuko News 

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages