TBL KUENDELEA KUUNGA MKONO KAMPENI ZA USALAMA BARABARANI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 1, 2021

TBL KUENDELEA KUUNGA MKONO KAMPENI ZA USALAMA BARABARANI

  Malunde       Wednesday, September 1, 2021

Mkurugenzi wa Uhusiano, Mawasiliano na Sheria wa TBL , Mesiya Mwangoka, akiongea wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani 
Kamanda wa kikosi cha Usalam barabarani, SACP Wilbrod Mutafungwa,akiongea wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani. Kulia ni Afisa Mnadhimu wa kikosi cha Usalama Barabarani ACP Mkadam Mkadam
Maofisa wa polisi wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani 
Maofisa wa Jeshi la Polisi na TBL katika picha ya pamoja baada ya mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani 

***

Kampuni ya TBL Plc imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, ulemavu na hasara mbalimbali.

Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani baina ya Maofisa wa kampuni ya TBL na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani wakiongozwa na Kamanda wa kikosi hicho, SACP Wilbrod Mutafungwa,uliofanyika jijini Dar es Salaam.

TBL Plc ni moja ya wadau wa kampeni za usalama barabarani nchini ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani kuendesha kampeni kwa madereva na watumiaji wa barabara kuzingatia sheria ili kupunguza matukio ya ajali nchini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post