DC MBONEKO ATEMBELEA MACHINJIO YA KISASA SHINYANGA , ASEMA MWAKA HUU LAZIMA KAZI IANZE


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, wapili kushoto, akikagua Marekebisho kwenye mradi wa Machinjio ya kisasa.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kutembelea mradi wa machinjio ya kisasa iliyopo Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ambayo imekuwa ikisuasua kukamilika, na kuahidi lazima mwaka huu ianze kazi ya kuchinja mifugo.

Mradi huo wa ujenzi wa machinjio ya kisasa Manispaa ya Shinyanga, ulianza mwaka 2018 na ulitakiwa ukamilike mwaka 2019, kwa gharama ya Sh. bilioni 5.57, lakini mpaka sasa haujakamilika, ambapo kila siku umekuwa ukifanyiwa marekebisho na kushindwa kukamilika.

Akiwa jana kwenye Machinjio hiyo, akiambatana na wataalam, pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, Mboneko alisema amechoshwa na kusuasua kukamilika kwa Machinjio hiyo na kuahidi kuwa lazima mwaka huu ianze kazi.

“Machinjio hii lazima mwaka huu ianze kazi ya kuchinja mifugo, tutakamilisha zile hatua ambazo ni muhimu zinazo ruhusu uchinjaji wa mifugo, ikiwamo kujenga mfumo wa majitaka,”alisema Mboneko.

“Machinjio hii itakapokamilika kwa hatua muhimu, tutazifunga machinjio zote za mjini hapa, ambazo zimeshachakaa na mazingira yake ya uchinjaji mifugo siyo wa kuridhisha,”aliongeza.

Naye Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, ambaye ndiye msimamizi mkuu wa ujenzi huo wa machinjio, alimhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa lazima adhima yake itimie ya Machinjio hiyo kuanza kazi mwaka huu, ambayo pia itakuwa ikichinja ng’ombe zaidi ya 100 kwa siku na mbuzi 500.

Kwa upande wake Mhandisi Erick Chunngu kutoka Kampuni ya GLISM ENGINERING ya Jijini Dar es salaam, ambapo wanafanya marekebisho ya machinjio hiyo, alisema kwa sasa wanaunganisha mfumo wa umeme kupeleka kwenye vyumba baridi, pamoja na kufanya marekebisho mengine, na watamaliza kabisa Septemba 30 mwaka huu.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye mradi wa Machinjio ya kisasa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, kulia, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kuwa machinjio hiyo lazima ianze kazi mwaka huu.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia), akiendelea na ukaguzi wa Marekebisho katika Machinjio ya kisasa.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kulia) akikagua Marekebisho kwenye mradi wa Machinjio ya kisasa.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akikagua Marekebisho kwenye mradi wa Machinjio ya kisasa.

Ukaguzi ukiendelea.

Muonekano wa Machinjio.

Ukaguzi ukiendelea wa mfumo wa Majitaka.

Mafundi wakiendelea na Marekebisho ya Machinjio hiyo.

Mafundi wakiendelea na marekebisho ya machinjio hiyo.

Na Marco Maduhu- Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments