Breaking

Post Top Ad

Monday, August 23, 2021

WAOMBAJI 68,019 WACHAGULIWA KUJIUNGA VYUO MBALIMBALI AWAMU YA KWANZA, DIRISHA AWAMU YA PILI KUFUNGULIWA AGOSTI 24


Waombaji  68,019  sawa na asilimia 73.2 ya waombaji  92,809, wamechaguliwa kujiunga katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa kozi za Shahada za kwanza kwa mwaka wa masomo 2021/2022.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa amesema ongezeko la waombaji limetokana na kuongezeka kwa wahitimu wa kidato cha sita.

Aidha Profesa Kihampa amesema dirisha la awamu ya pili la udahili linafunguliwa kesho Agosti 24,2021 mwaka huu hadi Septemba 6 mwaka huu, ili kutoa fursa kwa waombaji waliokosa nafasi kuomba katika awamu hiyo.

TCU imewataka waombaji kutuma maombi moja kwa moja katika vyuo, na kwa waombaji 35,548 waliochaguliwa chuo zaidi ya kimoja katika awamu ya kwanza ya udahili wanatakiwa kuthibitisha chuo kimojawapo katika vile walivyochaguliwa.

Majina ya waliochaguliwa chuo zaidi ya kimoja

 CLICK HERE TO DOWNLOAD PDF FILEDownload/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages