AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUUA MTOTO WA KAKA YAKE, KULA MAINI YAKE MANYARA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, August 22, 2021

AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUUA MTOTO WA KAKA YAKE, KULA MAINI YAKE MANYARA

  Malunde       Sunday, August 22, 2021

Mkazi wa Mtaa wa Silaloda Mji wa Mbulu mkoani Manyara, Harold Hhando anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kaka yake, Emmanuela Hhando (13) na kumtoa viungo vya mwili.

Inadaiwa Hhando alimuua mtoto huyo kwa kumpasua katikati ya miguu na kumtenganisha vipande viwili kisha kukata sehemu za siri, kumtoa maini na kutaka kuyapika ili ayale.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marrison Mwakyoma amesema tukio hilo lilitokea jana kijijini hapo.

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha tukio hilo ni ushirikina kwani Hhando ameeleza kuwa aliambiwa na mungu wake amuue mtoto wa kaka yake na kula maini ili avune mazao mengi.

Chanzo - Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post