ASKARI POLISI AMUUA KWA KUMPIGA RISASI MWENZAKE WAKIMKIMBIZA DEREVA WA LORI ALIYEGOMA KUSIMAMA Polisi wa kike kutoka kituo cha Polisi cha Gilgil Weighbridge kwenye barabara ya Ngong-Suswa amempiga risasi kimakosa afisa mwenzake wakimkimbiza dereva wa lori ambaye alikuwa amekataa kusimama licha ya kuamuriwa.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyorekodiwa Jumapili, Agosti, 22,2021 Emma Sopiato na wenzake walikuwa ndani ya gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin wakimfukuza dereva huyo wa lori ambaye alikuwa amekataa kusimama licha ya kuamuriwa.

 Hii ilipelekea mbio za paka na panya kati ya magari hayo mawili.

 Walipofika katika soko la Kimuka, dereva huyo wa lori alisimama na kisha alianza kurudi nyuma akiwa na nia ya kugonga gari la polisi.

 "Afisa huyo wa kike ambaye alikuwa ameketi nyuma ya dereva alitoa bunduki yake aina ya AK 47, ambayo ilimgonga koplo Fanuel Abongo, kwenye upande wa kulia wa mbavu zake na kutokea upande wa kushoto wa mbavu zake," ilisoma ripoti hiyo ya polisi.

Kisha Abongo alikimbizwa haraka katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Ngong na baadaye alihamaishwa hadi Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) kwa matibabu maalum.

 Kwa bahati mbaya Abongi akithibitishwa kuaga dunia alipowasili KNH. Maafisa wa upelelezi wameshikilia kuwa bado wanachunguza tukio hilo. 

Kulingana na ripoti ya polisi, bunduki ambayo ilitumika katika kisa hicho imewekwa chini ya ulinzi na mshukiwa amezuiliwa.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post