SIMBA SC YAPAA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA...YAITWANGA GWAMBINA FC 1-0 MISUNGWI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, April 24, 2021

SIMBA SC YAPAA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA...YAITWANGA GWAMBINA FC 1-0 MISUNGWI

  Malunde       Saturday, April 24, 2021

MABINGWA watetezi, Simba SC wamepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Gwambina FC Uwanja wa Gwambina wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki wa kushoto na Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein 'Tshabalala' aliyefunga dakika ya 29 kwa shuti la umbali wa mita 35 baada ya pasi ya kiungo Muzamil Yassin.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 24, ikiwazidi pointi moja vigogo, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi.

Tshabalala anafunga bao hilo siku mbili tu baada ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumia klabu hiyo hadi mwaka 2024.

CHANZO- BINZUBEIRY BLOG
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post