MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WAANDAMANA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, April 24, 2021

MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WAANDAMANA

  Malunde       Saturday, April 24, 2021

Baadhi ya mashabiki wa Manchester United walioandamana jioni ya leo wakiwa na bango lenye ujumbe wa kuwataka wamiliki wake waachie ngazi.
**
Licha ya wamiliki wa klabu ya Manchester United kuomba radhi siku chache zilizopita baada ya kukubali kushiriki kwenye michuano mipya ya European Super Ligi , lakini mamia ya mashabiki wa klabu hiyo wameandama jioni ya leo Aprili 24, 2021 kuutaka uongozi huo uachie ngazi.

Mashabiki hao wameandamana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza unaosomeka “Glazers Out. Edwoord ward Out” ukiwa na tafsiri ya kutaka wamiliki wao waachie ngazi pamoja na makamu mwenyekiti mtendaji Edwoord ward ajiengue.

Mgomo huo umekuja siku tatu baada ya klabu hiyo kutangaza kujitoa kwenye michuano hiyo mpya na wamiliki hao kuomba radhi kwa mashabiki kupitia vyanzo mbalimbali vya habari lakini mashabiki hao hawaoonekani kuridhishwa na namna klabu hiyo inavyoendeshwa.

Ikumbukwe kuwa, Jumapili ya Aprili 18, 2021 waandaaji wa michuano hiyo mipya kwa kushirikiana na benki ya Street Bank JP Morgan, waliorodhesha vilabu 12 vilivyothibtisha kushiriki mihchuano hiyo na klabu ya Manchester United ikiwemo.

Mashabiki hao mbali na kuwapinga wamiliki wa klabu hiyo, lakini wanapinga klabu yao kushiriki kwenye michuano hiyo kwasababu itaondoa msisimko na kuondoa mahusiano ya mashabiki na klabu yao hiyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post