JAJI MSTAAFU DKT. BWANA AHITIMISHA MKUTANO WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana akihitimisha Mkutano wa Tume namba 3 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, leo amehitimisha Mkutano wa Tume namba 3 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana amesema, katika Mkutano huu Tume imetoa uamuzi wa Rufaa 151 na Malalamiko 11 yaliyowasilishwa na watumishi mbalimbali wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Mamlaka zao za Ajira na Mamlaka za Nidhamu.

Kati ya rufaa 151 zilizotolewa uamuzi na Tume rufaa 82 zimekataliwa; rufaa 43 zimekataliwa kwa kuwa ziliwasilishwa nje ya muda uliowekwa kwa mujibu wa Sheria. Rufaa 12 zimekubaliwa; rufaa 11 zimekubaliwa kwa masharti kwamba zikashughulikiwe upya na Mamlaka zao za Nidhamu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Rufaa 3 hazikutolewa uamuzi kwa sababu ni  kesi zilizopo Mahakamani.

Kwa upande wa malalamiko, Tume ilipokea na kutoa uamuzi wa malalamiko 11 ambapo malalamiko 6 yamekataliwa, malalamiko 4 yamekubaliwa na lalamiko 1 limekataliwa kwa sababu liliwasilishwa nje ya muda. 

Imeandaliwa na:-

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Tume ya Utumishi wa Umma

DAR ES SALAAM

23 Aprili, 2021

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments