MHUNI ALIYEZOEA KUPAPASA WANAWAKE KWENYE MAGARI ASHAMBULIWA NYETI ZAKE BILA HURUMA

Jamaa mmoja mtaani Pipeline, Nairobi nchini Kenya anajuta kuumizwa sehemu zake za siri na kisura aliyejaribu kumdhulumu (kumshikashika bila ridhaa yake) wakiwa ndani ya gari la abiria daladala (Matatu). 

Duru zinaarifu kwamba jamaa huyo anajulikana na wengi kwa mazoea yake ya kuketi kando na akina dada garini na kuwapapasa huku akiwatolea kisu kuwatishia wasipige kelele.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, jangili huyo alikuwa akitekeleza haya majira ya usiku wakati taa zimezimwa kwenye matatu lakini jamaa hakujua kwamba chuma chake ki motoni.

 Siku ya kioja inasemekana kama kawaida lofa aliingia kwenye matatu na kuketi kando ya msichana mrembo ajabu. Safari ilianza huku muziki ukivuma garini kwa sauti ya juu hivi kwamba hakuna aliyemsikia mwingine.

Barobaro alijiandaa na kuupelekea mkono wake pole pole na kuuingiza kifuani kwa dada kisha akashika ziwa lake. 

Inasemekana wakati huu wote dada huyo alikuwa ametulia tuli naye jamaa akadhani ameangukia kivuno.

 Hata hivyo, alipokuwa amezubaa akiendelea na shughuli yake ghafla alishtuliwa na mkono wa kisura ukipenya katika zipu yake akadhani mrembo  alisisimuliwa na vioja vyake naye akamsaidia kuifungua zipu hiyo.

 Lo! Jamaa hakuamini kisura alipoing’ata sehemu yake ya siri na kucha zake refu na kuufinya bila huruma.

Inaarifiwa kuwa jamaa alijaribu kupiga nduru lakini sauti yake haikuweza kutoka. 

Hamna abiria mwingine yeyote aliyetambua kilichokuwa kikiendelea. 

Semasema zinaarifu kwamba jamaa aliinama kwa uchungu huku akitokwa kijasho lakini kisura hakumuonea huruma, mkono wake ulibaki palepale nusra kucha ziikate sehemu hiyo nyeti.

 Kisura alipokaribia kushuka ndipo aliachilia  lakini sehemu hiyo ilikuwa imepata majeraha mabaya.

 “Leo nafa jamani! Nani atanibeba kuelekea nyumbani?” jamaa aliuliza kwa sauti ya chini huku machozi yakining’inia machoni.

Jamaa aliposhuka stejini ilibidi aombe msaada na kwa bahati nzuri wakatokea wanaume wawili wasamaria wema ambao walimpeleka hadi kwa nyumba.

 “Kaka iwapo uliumia kazini, nenda hospitalini. Sehemu nyeti ni hatari zikiuma,” mmoja wa majamaa hao alimshauri. 

Penyenye zinaarifu kuwa jamaa angali anauguza majeraha nyumbani kwani anaogopa kwenda hospitalini kwa sababu itambidi aanike ukweli wa mambo yaliyomfika.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments