CHINA YALIPIZA KISASI CHA VIKWAZO KWA MAREKANI NA CANADA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, March 28, 2021

CHINA YALIPIZA KISASI CHA VIKWAZO KWA MAREKANI NA CANADA

  Malunde       Sunday, March 28, 2021


China imetangaza vikwazo dhidi ya Wamarekani wawili, raia mmoja wa Canada na Shirika la kutetea haki ili kujibu vikwazo vilivyowekwa mapema wiki hii juu ya inavyoshughulikia jamii ya Uyghurs. 

Wizara ya mambo ya nje ya China imewakataza, wajumbe wawili wa Tume ya Kimataifa ya Uhuru wa Kidini ya Marekani, Gayle Manchin na Tony Perkins, Mbunge wa Canada Michael Chong na Kamati ya Bunge ya Canada ya haki za binadamu kuingia China Bara, Hong Kong na Macau. 

Maafisa hao pia wamepigwa marufuku kufanya biashara na taasisi au raia wa China. 

Wizara ya mambo ya nje ya China imeishutumu Marekani na Canada kwa kuweka vikwazo kulingana na uvumi na habari ghushi.


DWUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post