RIPOTI YA CAG YABAINI DOSARI YA MATUMIZI YA FEDHA YANAYOFANYWA NA VYAMA VYA SIASA, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Bw. Charles E Kichere mara baada ya kumalizika kwa Hafla ya upokeaji wa Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20 na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai. Picha na Ofisi ya Rais
***

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kicheere imeendelea kubaini dosari ya matumizi ya fedha yanayofanywa na taasisi na mashirika ya umma pamoja na vyama vya siasa.

CAG amesema kati ya hati 900 alizozikagua, hati 800 sawa na asilimia 87 zinaridhisha huku hati 81 zikiwa na mashaka na mbaya ni 10.

Kichere ameyasema hayo leo Jumapili, Machi 28, 2021 wakati akikabidhi ripoti aliyoifanya kwa taasisi za Serikali Kuu, mamlaka ya serikali za mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na vyama vya siasa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ulioishia Juni 30, 2020.

“Tumeongeza mashirika 10 ambayo tunayakagua na nimeshirikiana na makampuni mengine binafsi kuhakikisha tunakagua ipasavyo pia tumefanya kaguzi za kitaalamu SGR, miundombinu mabasi yaendayo haraka, barabara kuu Morogoro, Kibaha, miradi ya maji wilaya ya Same na Korogwe,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments