NAIBU WAZIRI NDEJEMBI-SERIKALI KUANZISHA MPANGO WA KANZIDATA KWA WALENGWA WOTE WANAPOKEA FEDHA ZA TASAF KWENYE HALMASHAURI NCHINI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo bungeni

 

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia NGOs Mh .Neema Lugangira akiuliza swali bungeni

MWANDISHI WETU, DODOMA.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Mhe Deogratius Ndejembi amesema Serikali tayari imeanzisha kanzidata kwa walengwa wote wanaopokea fedha za TASAF ambao ulianza kwa Halmashauri 19 nchini lakini kwa sasa umekwisha kuzifikia Halmashauri 39.

Aliyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali mawili ya ya nyongeza ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia NGOs Mh Neema Lugangira ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuanzisha kanzidata kwa kutumia Tehama ili kuhakikisha wanufaika wa mpango wa TASAF ni wale waliokidhi vigezo ambavyo vimewekwa.

Sambamba na kuondoa mianya ya watu wanaonufaika na mpango huo kusajiliwa mara mbili kwenye maeneo tofauti tofauti jambo ambalo linapelekea wengine kukosa fursa hiyo muhimu.

Naibu Waziri huyo alisema pia wataanza kuweka mfumo wa kuunganisha kanzidata na NIDA na mitandao ya simu ili walengwa badala ya kupokea fedha dirishani kwa wale wanaoenda kugawa fedha hizo ziende moja kwa moja kwenye simu zao ili kuhakikisha hakuna malipo mara mbili.

Alisema kwa sababu kumekuwa na malalamiko kwamba watu wanapokea mara mbili fedha na hata mtu akiwa hayupo zinachukuliwa na watu wengine hivyo ili kudhibiti hilo lisiendelee kutokea ndio maana watakwenda kuweka mfumo huo kwenye Halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na maeneo ya Uguja na Pemba.

Katika swali lake la pili Mbunge Neema aliuliza Je serikali ina mpango gani kuhakikisha kaya ambazo hazikunufaika awali sasa zinanufaika kwenye awamu ya tatu ya TASAF hususani wazee sio tu kwa Manispaa ya Bukoba bali pia mkoa wa Kagera na Taifa kwa Ujumla.

Akijibu swali la pili la Mbunge huyo, Naibu Waziri huyo alisema Serikali itatanua mpango huu kwa wazee ambao hawakuingia na kaya ambazo hazikuingia wataingia hivyo aliwatoa mashaka wabunge wa majimbo na viti maalum nchini kuwa mpango huo unakwenda kwenye kaya milioni 1.4 ambazo ni sawasawa watu milioni 7 ambao watakwenda kunufaika na mpango huu wa TASAF.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments