KUTANA NA MREMBO ANAYEISHI MAKABURINI NA MPENZI WAKE

Mrembo Mghana kwa jina Abena amesimulia namna alifaulu kuishi miongoni mwa wafu katika Makaburi ya Osu jijini Accra, Ghana.

Katika mahojiano na EyeGhana ambayo tumeiona kwenye ukurasa wao rasmi wa YouTube, Abena alisema huwa ana uoga sana lakini hana budi ila kuvumilia hali ilivyo.

 Kulingana naye, alifanya uamuzi huo wa kuishi makaburini na mpenzi wake kwa sababu ya kushindwa kulipia makazi bora.

Abena, ambaye anaoneokana kuwa na miaka 20, alisema mara ya kwanza kuishi na mpenzi wake makaburini, alikuwa anahofia kuwa huenda baadhi ya wafu watafufuka kutoka makaburini.

Lakini mpenzi wake alimtia moyo kuwa jasiri na sasa akiwa na matumaini kuwa siku moja watahama na kuishi na watu wengine.

 "Lakini mpenzi wangu aliniambia nitakapokufa, pia mimi nitakuwa miongoni mwao kwa hivyo nisiogope kwa sababu hawapo tena na hawawezi kurudi," alisema Abena.

TAZAMA VIDEO HAPA AKIZUNGUMZA
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post