ACHOMWA KISU KISA SH. 1000 UGOMVI WA KUNG'ANG'ANIA KUCHEZA NA WASICHANA


Na Anthony Mayunga - Mwananchi
Mgusuhi Sabai anasakwa na polisi wilayani Serengeti mkoani Mara kwa madai ya kumjeruhi Silikale Mwita akipinga kutolewa katika sherehe ya harusi kwa kushindwa kulipa Sh1,000 ili aendelee kucheza muziki na wasichana.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyabirore kijiji cha Kenokwe, Chacha Zablon amesema tukio hilo limetokea  Jumanne Februari 9, 2021 saa 10 alfajiri nyumbani kwa Mang'o Kibuni aliyekuwa akimuozesha binti yake.

"Ukumbini huwa na wasichana wengi ambao wanaingia bure, wanaume wanatoa fedha ili waingie kucheza nao, humo ndani baadaye wanaanzisha mtindo wa kutoana kwa fedha kama njia ya kujiongezea kipato bibi harusi, na vijana kujionyesha kwa wasichana maana hiyo ni fursa ya kupata wachumba.”

"Sabai alitolewa kwa Sh500 ili kama ana Sh1000 abaki akataka kukaidi wakamtoa akawa amekasirika akitaka Silikale naye atoke kwa kuwa hakutoa fedha. Mzozo baada ya kupamba moto aliyejeruhiwa alitoka nje kumfuata mtuhumiwa ambaye alimchoma kisu tumboni,” amesema mwenyekiti.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post