RAIS WA ZANZIBAR, DK HUSSEIN ALI MWINYI KULIFUNGUA BARAZA LA WAWAKILISHI LEO | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, November 11, 2020

RAIS WA ZANZIBAR, DK HUSSEIN ALI MWINYI KULIFUNGUA BARAZA LA WAWAKILISHI LEO

  Malunde       Wednesday, November 11, 2020


Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi leo anatarajiwa kulifungua Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuanza kazi rasmi kwa miaka mitano ijayo.

Taarifa iliyosomwa jana na Spika wa baraza hilo, Zubeir Ali Maulid ilieleza Rais atalizindua baraza leo saa 9 alasiri.

Taarifa hiyo ilieleza kwa mujibu wa utaratibu, baraza hilo ili lianze kazi ni lazima kuzinduliwa na rais baada ya kukamilika kwa baadhi ya shughuli za kikatiba za baraza. Miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na kuchaguliwa kwa Spika na Naibu wake.

Kazi nyingine ni kuapishwa kwa wajumbe wa baraza waliohudhuria mkutano huo wakiwemo kutoka majimboni, wa viti maalum pamoja na walioteuliwa na Rais.

Katika kikao cha jana, kulifanyika uchaguzi wa Naibu Spika ambapo wajumbe wote 67 waliohudhuria walimchagua Mgeni Hassan Juma kwa kura zote za ndio.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post