IBRAHIM NGWADA AMECHAGULIWA KUWA MEYA WA MANISPAA YA IRINGA

 

Ibrahim Ngwada akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kuwa meya wa Manispaa ya Iringa

Na fredy Mgunda,Iringa.

Ibrahim Ngwada amechaguliwa Kuwa meya wa manispaa ya Iringa  kwa kupata kura 19 huku akifuatiwa na Jackson Chaula kwa kupata kura tano katika uchaguzi uliofanyika  ukumbi wa  chama cha mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo wa kumtafuta meya na naibu meya wa Manispaa ya Iringa Toviki Kivike alisema kuwa uchaguzi wa meya umefanyika kwa amani,uwazi na haki na wagombea wote wameridhika mara baada ya matokeo hayo kutangazwa.


Aidha msimamizi huyo alisema kuwa uchaguzi wa naibu meya ulifanyika mara mbili kutokana na ushindani ulikuwepo hivyo kuamriwa kurudia ndio alipopatikana mashindi.


Baada ya kutangazwa kuwa meya wa Manispaa ya Iringa  Ibrahim Ngwada  alisema kuwa anazitambua changamoto za wananchi wa manispaa za Iringa hivyo atahakikisha anazitatua vilivyo ili wananchi wapate maendeleo.

Ngwada aliongeza kwa kusema kuwa miaka mitano iliyopita Manispaa hiyo ilikuwa chini ya CHADEMA na walifanya maendeleo hivyoatakikisha wanafanya kazi kubwa kuleta maendeleo zaidi ya yaliyofanywa na watangulizi wake kuwa sasa manispaa hiyo ipo chini ya CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments