DONALD TRUMP ALALAMIKA KUIBIWA KURA....KASEMA ATAENDA MAHAKAMANI KUZUIA KUENDELEA KUHESABIWA KWA KURA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, November 4, 2020

DONALD TRUMP ALALAMIKA KUIBIWA KURA....KASEMA ATAENDA MAHAKAMANI KUZUIA KUENDELEA KUHESABIWA KWA KURA

  Malunde       Wednesday, November 4, 2020


Rais Donald Trump amedai kushinda uchaguzi wa Marekani licha ya kwamba matokeo ya mwisho bado hayajatangazwa, na amesema atakwenda Mahakama ya Juu kupinga kuendelea kuhesabiwa kwa kura. 

Trump amedai ushindi huo katika hotuba isiyo ya kawaida akiwa ikulu ya White House, na kuongeza kuwa kuendelea kuhesabiwa kwa kura ni njama ya kufanya udanganyifu. 

Mrepublican huyo ambaye matokeo ya awali yanamuonesha akiwa katika mchuano mkali na Mdemocrat Joe Biden, amesema atakwenda mahakamani na anataka upigaji kura wote kusimama - akionekana kumaanisha kusitisha kuhesabiwa kwa kura za posta, ambako kunaweza kuruhusiwa kisheria na bodi za uchaguzi za majimbo baada ya uchaguzi wa Jumanne iwapo zilikuja kwa wakati.

 Suala hilo linaweza kugeuka nyeti katika majimbo ambayo yanaendelea kuhesabu kura katika kinyang'anyiro hicho kikali. 

Timu ya kampeni ya Joe Biden imekosoa matamshi hayo ya Trump na kuyataja kuwa kashfa, na baadhi ya wanachama wa chama chake cha Repulican pia wameikosoa hatua hiyo.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post