DC KISWAGA: BAADA YA UCHAGUZI TUGEUKIE KILIMO


Samirah Yusuph,
Bariadi. Baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi mkuu na hatmaye kupatikana kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, wabunge pamoja na madiwani, wananchi wameshauriwa kugeukia shughuli zao za kiuchumi.
 
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake.

Ambapo wananchi wametakiwa kujikita katika shughuli zao za kila siku ili kujiongezea kipato kwani sasa ni msimu wa kilimo na wakati wa maisha baada ya uchaguzi hivyo ni muda kuendelea na shughuli za kilimo.

Huku akiwataka wananchi kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kulima zao la Pamba kwa wingi kutokana na taarifa za mamlaka ya hali ya hewa kutoa taarifa ya uwepo wa mvua chache kwa mwaka huu.

Kiswaga alisema msimu wa mvua chache ni msimu mzuri kwa wakulima wa zao la Pamba kwani uzalishaji wake unakuwa ni mkubwa kutokana na zao hilo kutokuhitaji mvua nyingi hivyo wananchi watumie nafasi hiyo katika kuongeza uzalishaji na kuongeza kuwa:

"Tayari pembejeo za kilimo cha pamba zimefika katika ofisi za ushirika hivyo wananchi wafike kwa ajili ya kuchukua mbegu ili kazi iendelee kama kawaida".
 
Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post