CHADEMA WAMUUNGA MKONO MAALIM SEIF

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kumuunga mkono Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na kuachiana majimbo na kata na chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Uamuzi huo umetangazwa leo Jumapili tarehe 4 Oktoba 2020 na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema wakati anatangaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho, iliyoketi jana Jumamosi jijini Dar es Salaam.


Mbowe amesema, uamuzi huo umekuja baada ya  Mgombea Urais wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohammed kuridhia kujitoa katika kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono Maalim Seif.


Mbowe amesema, Kamati Kuu za Chadema na ACT-Wazalendo ziko katika utaratibu wa kutafuta namna watakavyoshirikiana katika Uchaguzi wa wabunge na madiwani kwa pande zote mbili, Tanzania Bara na Zanzibar.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments